
Kikosi cha Majimaji FC.
Ushindi huo
umeifanya Simba SC kufikisha jumla ya Point 35 na kuendelea kuongoza Ligi kwa
kufikisha Jumla ya Point 35 wakifuatia na Azam FC wenye Point 30 huku Singida
United baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons wamesogea nafasi ya
nne kwa kufikisha Point 27.
|
![]() |
Mshambuliaji
wa Simba SC,John Bocco Jana Januari 28, 2018 amefunga magoli mawili dhidi
ya Majimaji FC na kufikisha magoli saba (7) kwenye msimu huu wa Ligi 2017/2018 ambapo
raundi ya kwanza imemalizika baada ya kila timu kucheza mechi 15.
Katika mechi
za hivi karibuni Bocco amefunga magoli muhimu ambayo yaliamua baadhi ya mechi,
(Tanzania Prisons 0-1 Simba SC, Ndanda FC 0-2 Simba SC, Simba SC 4-0 Majimaji
FC ) Bocco amefunga mabao matano katika mechi hizo ambazo Simba ilifunga magoli
saba.
Mshambuliaji
huyo wa Simba SC ameungana na Obrey Chirwa (Yanga SC) Mohamed Rashidi (Tanzania
Prisons) na Habib Kiombo (Mbao FC) wote wakiwa wamefunga magoli saba.
|

No comments:
Post a Comment