
Nteghenjwa
Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna
wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa
kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga
madarasa bora.
Waziri Jafo
ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na
Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa
ufanisi.
“Viongozi
wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie
kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye
mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe,
mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa
bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi
watajiskia fahari kusoma”Alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo
hakusita kuwakumbusha Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu
ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini.
Niwapongeze
baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi
wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi na wamejenga
mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30
April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya
iwe imekamilika.
Waziri Jafo
alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya
kuheshimu mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini, kutunza Siri za
Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Awali
akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa mafunzo haya yanakamilisha
mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane iliyopita na baada ya
mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia Viongozi 324.
Prof.Semboja
aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo yamelengwa
tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo wa kufanya
maamuzi wa Kimkakati kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kwa manufaa mapana
ya sasa nay a baade ya Jamii Tunayoihudumia.
Sambamba na
hilo Mkutano huu pia unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi wetu katika kuongoza
watu na rasillimali zingine zilizoko kwenye maeneo yetu ili kwa pamoja tuweze
kufikia malengo ya pamoja.
Alisisitiza
kuwa Mafunzo haya yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa Binafsi za
Viongozi kwa sababu Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi katika kiLA
Eneo hivyo ni lazima kila kiongozi aweze kujitenegenezea Sifa binafsi ili
akubalike na kuhesimika katika Jamii husika.
“Sifa hizi
binafsi tunazozizungumzia ni Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu, Mtenda Haki,
Muumini wa Utawala bora na Utawala wa Sheria na zaidi kuwa mchahapa kazi na awe
na weledi wa hali ya juu sasa haya yote yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya
namna gani Kiongozi anaweza Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii
tunazoziongoza.
Akitoa Neno
la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya Mkuu wa
Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI na Taasisi ya
Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi ameahidi Umakini wa washiriki kwa
siku zote za mafunzo.
Mafunzo haya
ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa imegususa Viongozi kutoka katika Mikoa ya Mtwara, Lindi,
Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
No comments:
Post a Comment