UEFA 2017/2018- Man U sasa Alama 12 Kundi A. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 01, 2017

UEFA 2017/2018- Man U sasa Alama 12 Kundi A.


Manchester United ikiwa nyumbani katika dimba la Old Trafford imefanikiwa kuichapa Benfica 2-0 na kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne inaweza kuingia katika hatua ya mtoano.
Man United ambayo imeingia katika mashindano hayo kwa kuchukua kikombe cha ligi ya Europa msimu uliopita  2016 /2017 wameshinda michezo yote minne waliocheza na hivyo wanahitaji alama moja pekee katika michezo miwili iliyosalia ili kuweza kufuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.

Mchezaji Daley Blind akipongezwa na wachezaji wenzake wa Manchester United, Scott McTominay (kulia) na mshambuliaji Romelu Lukaku (kushoto), baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwa penalti 78 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Benfica kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana October 31,2017 Uwanja wa Old Trafford.


Goli la kwanza Benfica walijifunga kupitia kwa kipa wao, Mile Svilar dakika ya 45 kufuatia shuti la Nemanja Matic  



Kwa matokeo hayo Man Uited inaongoza ikiwa na alama 12, huku Benfica ikiburuta mkia na alama 0.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad