Bayern Munich na PSG zakwanza Kufuzu 16 Bora ya Michuano ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ 2017/2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 01, 2017

Bayern Munich na PSG zakwanza Kufuzu 16 Bora ya Michuano ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ 2017/2018.


Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani na PSG ya Ufaransa zimekuwa timu mbili za kwanza kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ‘UEFA’ msimu huu wa 2017/2018.

Timu hizo zimefuzu baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yake ya kundi B usiku wa kuamkia leo ambapo PSG wakiwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Anderlecht ya Ubeligji.


Baada ya ushindi huo PSG sasa imefikisha alama 12 na kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora kutokana alama zake kutofikiwa na timu mbili za mwisho kwenye kundi B ambazo ni Celtic na Anderlecht.

Kwa upande mwingine Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich nao wametinga hatua ya 16 bora kutoka Kundi B baada ya kujikusanyia alama 9 nyuma ya PSG hivyo kuzitupa nje timu za Celtic na Anderlecht

Bayern imeifunga Celtic mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo.

Ligi hiyo ya mabingwa barani Ulaya itaendelea leo Jumatano November 01,2017 kwa michezo nane kutoka kwenye makundi manne kupigwa ambapo mabingwa watetezi Real Madrid watakuwa nchini England kucheza na Tottenham Hospurs.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad