Bodi ya Ligi
Tanzania TPLB imetoa kibali rasmi kwa klabu ya soka ya Singida United kuanza
kutumia uwanja wake wa Namfua kama uwanja wa nyumbani kwenye mechi zake za ligi
kuu msimu huu.
Bodi
imeziandikia barua timu zote 16 za ligi kuu kuzifahamisha juu ya Singida United
kuhama kutoka uwanja wa Jamhuri Dodoma ambao ilikuwa inautumia kama uwanja wake
wa nyumbani na sasa itarejea Singida kwenye uwanja wa Namfua.
Uwanja huo
wa Namfua utaanza kutumika Jumamosi hii Novemba 4 kwenye mchezo wa Ligi kuu
soka Tanzania bara raundi ya 9 ambapo Singida United itacheza na mabingwa
watetezi Yanga SC.
Singida
United wamewaaga rasmi mashabiki wao wa mkoani Dodoma na kuwatakia kila
la kheri na timu yao ya Dodoma FC wakiwaombea ipande daraja ili mwkaani waweze
kushuhudia uhondo wa Ligi Kuu.
|
No comments:
Post a Comment