Siku sita
baada ya Adam Malima kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mahakama imemfutia
kesi ya shambulio iliyokuwa ikimkabili.
Rais John
Magufuli, Alhamisi Oktoba 26,2017 alifanya uteuzi mbalimbali ukiwemo wa Wakuu
wa Mikoa.
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Novemba 1,2017 imeifuta kesi dhidi ya Malima
na mwenzake.
Malima
ambaye amesharipoti mkoani Mara hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo
ukitolewa.
Hakimu Mkazi
Mkuu, Respicius Mwijage ameifuta kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa baada
ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe.
Chini ya
kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Mutalemwa ameomba shauri
lifutwe kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka
dhidi ya washtakiwa.
Baada ya
ombi hilo kuwasilishwa, Hakimu Mwijage alimuhoji Mutalemwa iwapo kuna sababu ya
kuifuta kesi hiyo na kama hana hataifuta.
Wakili Mutalemwa
alisoma kifungu hicho akisema kinampa mamlaka DPP kuiondoa kesi mahakamani
wakati wowote anapoona inafaa na pia, kinamruhusu kuirudisha mahakamani.
Baada ya
maelezo hayo, Hakimu Mwijage alikubali kuwaachia huru washtakiwa.
Shauri hilo
lilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka.
Waliposomewa
maelezo ya awali, Malima na mshtakiwa mwenzake Ramadhani Kigwande walikubali
maelezo yao binafsi, siku ya tukio walikuwepo Masaki, walikamatwa na
kushtakiwa.
Walikana
maelezo mengine kuhusu mashtaka yanayowakabili.
Katika kesi
hiyo, Malima aliyewahi kuwa naibu waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na
mbunge wa zamani wa Mkuranga alidaiwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa
makusudi alimzuia ofisa wa polisi Konstebo Abdu kufanya kazi yake halali.
Malima
alidaiwa kumzuia askari huyo kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la
kumshambulia Mwita Joseph.
Kigwande
alidaiwa Mei 15,2017 eneo la Masaki wilayani Kinondoni akiwa na nia ya kumzuia
Mwita Joseph, ambaye ni ofisa operesheni wa kampuni ya Priscane Business
Enterprises alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari alimshambulia na
kumsababishia maumivu.
Waliposomewa
mashtaka, washtakiwa walikana na walikuwa nje kwa dhamana kwa kila mmoja
kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini bondi ya Sh5 milioni.
|
No comments:
Post a Comment