Vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango
wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita.
|
|
(PICHA NA JUMAPILI MAGESA)
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya
Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa
vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert
Gabriel alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika
ujenzi wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo.
" Inashangaza sana kuona maeneo mengine
wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja
lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha
katika miradi ya Serikali"Alisema Lughumbi.
Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia
vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa
madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye
fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii.
Katika hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa
Shule ya Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa miundombinu
hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka.
Aidha, ameagiza shule hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo
vilivyojengwa vianze kutumika badala ya kufungwa.Pamoja na kutembelea Shule ya
Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea shule ya Sekondari na kukagua
ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo.
Shule ya Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia
shilingi milioni 13 kwa kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya
kisasa pamoja na ukarabati wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na
fedha iliyobaki katika bajeti ya darasa moja.
Mkoa wa Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali
imeandaa mpango kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na jamii na
wadau wote wa Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
|
No comments:
Post a Comment