![]() |
|
Kabla ya
Utenguzi huo, Rais John Magufuli aliwabana wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
na Manispaa ya Bukoba akitaka kujua matumizi ya fedha za mfuko wa barabara
zilizopelekwa huku baadhi ya viongozi wakishindwa kutoa majibu.
Akizungumza
leo Novemba 6 ,2017 wakati wa uzinduzi
wa mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera Rais Magufuli
amesema anashangazwa kuona viongozi aliowateua wanakosa majibu juu ya fedha za
Serikali.
“Serikali
huwa inaleta fedha kwaajili ya maendeleo ya kila manispaa na hata hapa
tumeshaleta,”
“Mkurugenzi
wa Manispaa,tumeleta kiasi gani hapa? bajeti ya manispaa ya Bukoba ni kiasi
gani?amehoji na kwamba anataka watu wajue matumizi yake.
Mkurugenzi
wa manispaa hiyo Erasto Mfugale , amemueleza kuwa hadi sasa amepokea Sh33
bilioni ikiwa ni bajeti ya jumla huku akishindwa kutolea majibu fedha za mfuko
wa barabara.
“Katika fedha hizo kuna fedha ambazo ni
mishahara ambazo ni mishahara Sh19 bilioni kwa mwaka,”amesema
Kabla
hajamaliza, Rais alimuuliza “fedha za road fund (mfuko wa barabara)ni kiasi
gani, nasema hivi kwasababu zinapoteaga poteaga tu nataka uziseme
hapahapa,”amesisitiza
Mkurugenzi
huyo ameshindwa kutoa majibu suala ambalo rais ameliita ni kucheza na fedha za
Serikali.
Naye
Mkurugenzi wa halmashauri, Mwantum Dau alivyosimama kutoa majibu alisema
hakumbuki ni kiasi gani suala ambalo limeonekana kumkasirisha rais.
“Hapana
mheshimiwa Rais labda aje mtunza hazina, mimi nina idara nyingi siwezi
kukumbuka,” alisema
Rais amesema
anashangaa kuona viongozi aliwateua hawajui kuhusu fedha za Serikali.
“Nani
anafahamu hela za mfuko wa barabara manispaa ya Bukoba kwa sababu viongozi
niliowateua hawajui,pengine naweza nikateua Mkurugenzi sasa hivi,”amesema
Meya wa
Manispaa hiyo Jerry Silaa ndiye aliyewanasua viongozi hao baada ya
kueleza jumla ya fedha Shmilioni700 za ujenzi wa barabara pamoja na Sh120
kwaajili ya maboresho.
|








No comments:
Post a Comment