![]() |
|
Tatizo
alilozaliwa nalo Nathan kitaalamu linaitwa Tbilateral Proximal Femoral Focal
Deficiency (TPFD) ambapo watu 25 tu duniani ndio wamezaliwa na tatizo hilo.
Kati ya watu
hao 25 ni yeye pekee ndiye aliyefanikiwa kutembea ingawaje anapata changamoto
kubwa ya kusuguana kwa mifupa kwenye eneo la kiuno.
“Nasikia
kuna watu 25 tu hapa duniani wenye hali kama yangu lakini ni mimi pekee mwenye
uwezo wa kutembea hilo jambo linanifanya nijione mwenye bahati.
Ingawaje sio
kwa umbali mrefu wala sio kila siku lakini kwani nikifanya hivyo huwa napata
maumivu makali kiunoni kwani kuna msuguano kati ya mifupa ya miguu na kiuno.”amesema
Nathan kwenye mahojiano yake na Daily Mail.
“Sijioni
kama nina utofauti mkubwa na wenzangu, ingawaje kila ninayekutana naye kitu cha
kwanza anaangalia ulemavu wangu na mimi sijali hilo. Kwa sababu ulemavu
haunielezei mimi jinsi nilivyo moyoni“amesema Nathan.
Tazama Picha
za wawili hao jinsi walivyopendeza.
|










No comments:
Post a Comment