|
Katika semina hiyo wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitoa
changamoto zao katika kuendesha biashara za mafuta ikiwa ni pamoja na EWURA na
Mamlaka nyingine kuchelewesha taratibu
za utoaji wa vibali vya kuanzisha vituo vya mafuta ambapo vibali hivyo huchukua
muda mrefu zaidi ya mwaka tangu mwombaji aombe kupata leseni.
Akitoa majawabu ya changamoto hiyo Mhandisi Samweli alisema
kuwa tayari Mamlaka (WEWURA) wamekaa na wadau wengine kama NEMC wanaohusika na
usimamizi wa mazingira na kuwekeana mkakati wa kuhakikisha utoaji wa vibali unakwenda
haraka ili kutowakwamisha wafanyabiashara , mfano kwasasa (EWURA) wanashughulikia leseni kwa siku 45 tu kama mwombaji atakuwa ametimiza
vigezo vyote.
Wafanya biashara walioshiriki katika semina hiyo waliishukuru
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuwapa elimu juu ya
sheria na kanuni za kuendesha biashara zao hasa uanzishwaji wa vituo vya mafuta
kwani walikuwa wanapata changamoto hasa maeneo ya kuweka vituo vya mafuta kwani kabla ya semina walifikiri kuwa vituo
havitakiwi kuwekwa karibu na makazi ya wananchi.
|
|
Pongezi hizo zilitolwa baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
EWURA Mhandisi Godwini Samwel kutoa ufafanuzi kuwa hakuna sheria inayozuia kituo cha mafuta
kujengwa karibu na makazi ya wananchi ispokuwa taratibu zote za usalama
zikifuatwa. Pili alisema kuwa Vituo vya mafuta vinajengwa ili kuwahudumia
wananchi kwahiyo ni bora vikawa karibu na wananchi ambao wanategemea kupata
huduma hiyo.
Akifunga Semina hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Oktoba 9, 2017 Afisa
Biashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Isaya tendega alitoa wito kwa wafanyabiashara wa
Kagera kuhudhuria semina kama hizo zinzpoitishwa na kusisitiza kuwa zina manufaa
makubwa katika uendsha ji wa biashara ya mafuta na zinawapunguzia faini
wafanyabiashra zisizokuwa za lazima.
Aidha, Bw. Tendega aliwashauri wafanyabiashara waliohudhuria
wanaporudi makazini kwao wawaelimishe waenzao kwa kuwapatia makabrasha
waliopewa katika semina hiyo ili wayasome na kuzijua Sheria na kanuni za uendeshaji
wa biashara za mafuta ili mkoa uwe na
wafanyabiasha walio rasmi na kuondokana na biashara zisizorasmi.
Hadi sasa Mkoa wa Kagera una wafanyabiashara au wauzaji wa
mafuta ambao ni rasmi wenye vituo 48 na wauzaji wasio rasmi 72. Jumla ya
wafanya biashara ya mafuta yaani wauzaji ambao ni rasmi na wasiokuwa rami jumla
ni 120.
Kati ya wadau waliopongezwa kwa kufuata sheria, Kanuni na
taratibu za kuanziasha na kutoa huduma za biashara ya mafuta
Mkoani Kagera ni Bw. Remigius Patrick (Maarufu kama Dk Remy) mwenye kituo cha
Smart Oil Kibeta Manispaa ya Bukoba wafanyabiashara wameaswa kuiga mfano wake.
|





No comments:
Post a Comment