Taswira Picha -Ngara ilivyotamba Katika Mchezo wa Kuvuta Kamba ,Kukimbiza Kuku na Kukimbia kwenye Gunia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 09, 2017

Taswira Picha -Ngara ilivyotamba Katika Mchezo wa Kuvuta Kamba ,Kukimbiza Kuku na Kukimbia kwenye Gunia.

Timu ya Wanawake ya mchezo wa Kuvuta Kamba ya Ngara ikishangilia baada ya kuibuka washindi dhidi ya wenzao wa Giterenyi.Wilaya ya Ngara ,mkoani Kagera nchini Tanzania Jana October 08,2017 imesafiri na Viongozi wake baadhi wa Halmashauri hiyo kwenda wilayani  Giteranyi mkoa wa Muyinga nchini Burundi kucheza michezo mbalimbali na wenyeji wao katika uwanja wa Giteranyi ambapo lengo la ziara hiyo ilikua ni kukuza Upendo,Mshikamano na Ujirani mwema wa Wilaya hizo kupitia Michezo.
Timu ya Wanawake ya Ngara ,mkoani Kagera na wenzao wa Giterani Mkoani Muyinga nchini Burundi wakichuana katika mchezo wa kuvuta kamba Jana October 08,2017 Mjini Giteranyi.

Katika ziara hiyo ;Ngara walifanikiwa Kushinda mchezo wa Kuvuta kamba Wanaume kwa Alama 2 dhidi 1 ya Giteranyi-Burundi  huku Wanawake Ngara wakishinda nao kwa Alama 2 -0.

Mchezo wa  Kufukuza Kuku mshindi waliibuka Ngara  kwa Msichana kumchukua Kuku wakati kwenye Kukimbia kwenye Magunia Wanaume mshind wa Kwanza na wa Pili walitoka Ngara  huku Kukimbia kwenye Magunia Wanawake Mshindi wa Kwanza alitoka Ngara.


Timu ya Basketball  ya Ngara ,mkoani Kagera wakipasha kabla ya kuja kufungwa na Giteranyi Vikapu 10 -0 Jana October 08,2017 Mjini Giteranyi.

Mashabiki wengi walijitokeza kufatilia michezo mbalimbali kwa Timu ya Ngara ,mkoani Kagera na kupambana na wenzao wa Giterani Mkoani Muyinga nchini Burundi Jana October 08,2017 Mjini Giteranyi.


Timu ya Giteranyi FC ya  Mkoani Muyinga nchini Burundi wakicheza uwanja wao wa Nyumbani walifanikiwa kuwafunga Ngara Stars kwa bao 2-1.


Dr David Mapunda (kushoto) toka  Idara ya Afya Ngara ,mkoani Kagera akifatilia mchezo wa soka na wenzake wakati Giterani FC ya wilayani humo ikicheza dhidi ya Ngara Jana October 08,2017 Mjini Giteranyi.



Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngara ,mkoani Kagera Aidan Bahama (Mkuu wa Msafara wa ziara hiyo )akifatilia mpambano mkali wa soka kwenye uwanja wa Giterenyi akiwa na Mkuu wa wilaya ya Giteranyi Mkoani Muyinga nchini Burundi, Bi.Florida Shimilimana ( kulia).






Katika michezo mingine ya  Volleyball,Basketbal  na Soka, Ngara na  haikufanya vyema baada ya kuchakazwa michezo hiyo  bila huruma kwa soka kuchapwa 2-1 na Giteranyi.

Akizungumzia Matokeo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,Aidan Bahama amefafanua  kuwa  Changamoto kwenye michezo ya Volleyball,Basketball ni kutofanya mazoezi, kukosa pumzi pamoja na Stamina na kuwataka wanamichezo wilayani humo kuwa mazoezini wakati wote ili wanapoingia kwenye mashindano yoyote waweze kuleta ushindani.

Nae Afisa Michezo wilaya ya Ngara ,Said Salumu amesema kuwa watajipa upya kwa timu zilizofanya vibaya kwenye ziara hiyo kwani mchezo wowote ni mchezo wa  makosa yaani ukikosea Mwenzio anakufunga.
Aliyesimama ni cha mkuu wa Timu ya Giterani FC ya Giteranyi ,Mkoani Muyinga nchini Burundi.

Seleman Ally Kocha mkuu wa imu ya Ngara Stars ya Ngara ,mkoani Kagera nchini Tanzania.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad