VPL 2017/2018 -Asilimia 90 ya Sare zatawala Mechi za Leo September 30 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 30, 2017

VPL 2017/2018 -Asilimia 90 ya Sare zatawala Mechi za Leo September 30 .

Wenyeji Yanga SC wameendeleza mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/2018 baada ya jioni ya leo September 30,2017 kulazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Sare hiyo inaifanya Yanga ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tano, ikishinda mbili na kutoa sare tatu, wakati Mtibwa inafikisha pointi 11 baada ya sare hiyo ya pili, ikiwa pia imeshinda mechi tatu.
Ni mechi ya tatu Yanga wanatoka sare katika ligi ikiwa ni mechi ya tano tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Wanajangwani walitoka sare kwa mara ya kwanza dhidi ya Lipuli kwenye mechi ya ufunguzi walipolazimisha sare ya kufungana 1-1.
Mechi za leo  sare zimetawala kwa asilimia 90 katika Katika mechi saba zilizochezwa leo ni mechi moja tu ambayo kumekuwa na ushindi huku sita zote zikiwa ni sare.

Mechi pekee iliyokuwa na ushindi ni ile Ndanda FC ikiwa nyumbani imefanikiwa kuiripua Lipuli kwa mabao 2-1.

Lakini nyingine sita, sare zimechukua nafasi ukianza na sare ya 0-0 kati ya Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar.

DODOMA:

Azam FC ikiwa ugenini dhidi ya Singida United, imelazimisha sare ya 1-1 baada ya kusawazisha.

MWADUI:

Nayo Mwadui FC ikiwa nyumbani iemshindwa kuulinda ushindi wake kwa kuiachia Mbeya City isawazishe na matokeo kuwa 2-2.

MWANZA:

Pamoja na kuonyesha wako vizuri, Mbao FC nao wameokoka wakiwa nyumbani CCM Kirumba baada ya kusawazisha katika mechi dhidi ya Prisons iliyotangulia kufunga. 

Dakika 90 zimeisha 1-1.

SONGEA:

Majimaji wakiwa kwenye Uwanja wa nyumbani wa Majimaji mjini Songea wametoka uwanjani kwa sare ya 0-0 dhidi ya Kagera Sugar.

PWANI:

Ruvu Shooting walio nyumbani, nao wameshindwa kupata ushindi baada ya Njombe Mji kuamka na kusawazisha na matokeo ya dakika 90 yakawa 1-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad