EPL 2017/2018- Manchester United na Tottenham wapiga 4G. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 30, 2017

EPL 2017/2018- Manchester United na Tottenham wapiga 4G.

Manchester United waliokuwa nyumbani Old Traford Leo September 30,2017 dhidi ya Crystal Palace ambapo sekunde 180 tu zilimtosha Juan Mata kufunga bao la kwanza kwa United ikiwa pia ni bao lake la kwanza katika msimu huu wa EPL.

Marouane Fellaini aliongeza mawili kabla Lukaku kufunga la nne na kuifanya timu hiyo kushinda magoli manne kwa mara ya 3 msimu huu huku msimu uliopita walishinda magoli manne Old Trafford mara moja tu.

Goli alilofunga hii leo Romelu Lukaku lilikuwa bao lake la 7 katika michezo yake 7 ya mwanzo ya Epl na kumfanya kufikia rekodi hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa ikishikiliwa na Andy Cole.

Swansea waliendelea kupigika baada ya leo kuchezea kichapo cha bao 1 kwa sifuri toka kwa West Ham huku West Bromich na Watford wakienda sare ya bao mbili kwa mbili, Stoke City nao wakiwa nyumbani waliichapa Southampton bao 2 kwa 1.
Tottenham wameweka rekodi mpya katika Epl kwa kushinda michezo 6 mfululizo ya ugenini baada ya hii leo September 30,2017 kuibuka tena kidedea kwa ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Huddersfield.

Mabao mengine ya Tot yaliwekwa kimiani na Ben Davies huku Moussa Sissoko akifunga bao lake la kwanza katika michezo 44 tangu ajiunge na Tottenhma Hotspur.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad