|
Klabu ya
Simba, Jumatatu September 04,2017 imeitangaza Kamati Maalum itakayohusika na
kumtafuta mzabuni ambaye atanunua hisa 50% za timu hiyo katika suala lake la
uendeshaji mpya wa klabu hiyo.
Kamati hiyo
itaundwa na Wajumbe watano na itaongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu,
Thomas Mihayo sambamba na wajumbe wanne ambao ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge
wa Ilala, Azzan Zungu, Yussuf Majjid Nassor na Abdulrazak Badru ambaye ni
Mkurugenzi wa Bodi ua Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania.
Kamati
itakutana Alhamisi wiki hii kuanza kazi ya kuwajadili wanachama ambao watataka
kuzinunua hisa hizo ambapo watafuata sheria za manunuzi ya umma ambapo watakaa
kwa siku 45 kabla ya kumtangaza mzabuni wa timu hiyo.
|
No comments:
Post a Comment