Ilikuwa ili
kuvunja rekodi lazima kuogelea mara ya tatu .
Mamia ya
waogeleaji waliokuwa utupu walijumuika kwa pamoja kuogelea katika mto wenye
maji baridi katika jaribio la kuvunja rekodi nchini Finland.
Washiriki
walikuwa wanataka kuvunja rekodi ya dunia ya watu wengi zaidi kuwahi kuogelea
kwa pamoja wakiwa utupu.
Watu 789
waliokuwa pia wanahudhuria tamasha ya muziki mashariki mwa Finland walijitosa
kwenye maji kuogelea wakiwa utupu, waandalizi wanasema.
Walifanikiwa
kuvunja rekodi ya awali iliyokuwa imewekwa na waogeleaji nchini Australia, kwa
kuzidi watu hao kwa watu watatu, taarifa zinasema.
Waandalizi
wamesema sasa wanasubiri rekodi yao ithibitishwe na maafisa wa Guinness World
Records.
Hii ni mara
ya tatu kwa jaribio la kuvunja rekodi hiyo kuandaliwa nchini Finland, mtandao
wa habari wa Yle umesema.
Rekodi
waliokuwa wakijaribu kuivunja iliwekwa mwaka 2015 mjini Perth na watu 786
waliokuwa wanajaribu kuhamasisha watu kuipenda miili yao.
Kuogelea nje
kwenye mito na bahari ni utamaduni wa miaka mingi nchini Finland, ambapo
"avantouinti" - kuogelea katika shimo la barafu - hutangazwa na bodi
ya utalii nchini humo kama shughuli inayosaidia kusisimua mwili.
|
No comments:
Post a Comment