Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga
kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa
katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
washabiki waliohudhuria mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga
katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mpira
pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela katika uwanja wa Nyamagana ambapo
timu ya Buhongwa United ilikuwa ikicheza na Nyamwaga FC.
|
Rais John
Magufuli anazindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani
Sengerema hapo kesho July 04,2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Bw.Emmanuel
Kipole amesema kuwa Rais Magufuli atafika Wilayani hapo kwa ajili ya uzinduzi
huo.
Mradi huo
ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh bilioni 23 utawanufaisha
zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo 13,000 ambapo amesema wilaya hiyo ina jumla ya
wakazi 74,186 kutokana na Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2002 hivyo mradi huo
kwa sasa utahudumia kata 11.
|
No comments:
Post a Comment