*YALIYOJIRI
BUNGENI KATIKA KIKAO CHA 58 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 03 JULAI,
2017*.
1.Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) ndiyo yenye jukumu kuu kisheria la kukusanya mapato ya
Serikali.
2.TRA
ilianza rasmi kukusanya kodi ya majengo kwa Halmashauri 30 kati ya 183 kuanzia
Octoba 2016.
3.Katika
kipindi cha Julai-Septemba, 2016,Halmashauri 30 ziliweza kukusanya shilingi
milioni 3,399 sawa na asilimia 24 ya lengo la kukusanya milioni 14,502.
4.Kati ya
Octoba 2016 hadi Aprili 2017, jumla ya Shilingi Milioni 10,652.6 zilikusanywa
sawa na aslimia 22.0 ya lengo la kukusanya Shilingi Milioni 48,340.2.
5.Ufanisi
huu ni sawa na wastani wa makusanyo ya Shilingi Milioni 1,521.8 kwa mwezi.
6.TRA
imekusanya kodi ya majengo kwa ufanisi zaidi ikilinganishwa na Halmashauri.
7.Serikali
imeaainisha maeneo yote nchini yanayofaa kwa Kilimo cha umwagiliaji na kuandaa
Mpango Kabambe wa kuendeleza Kilimo cha umwagiliaji.
8.Mpango huu
utahusisha matumizi ya maji ya maziwa makuu ikiwemo Ziwa Victoria kwa ajili ya
umwagiliaji wa kutumia teknolojia zinazotumia maji kwa ufanisi.
9.Awamu ya
tatu ya Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) umeanza kwa Nchi nzima tangu
Mwezi Machi, 2017.
10.Serikali
imeweka utaratibu ambapo posho za viongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji
zinalipwa na Halmashauri kupitia asilimia 20 inayotengwa kutokana na mapato ya
ndani ya Halmashauri na kurejeshwa kwenye Vijiji.
11.Serikali
inakusudia kuliweka kwenye Sheria ya Fedha suala la kutenga asilimia 20 kama
posho za viongozi wa Serikali.
12.Serikali
imetenga Shilingi Milioni *557.3* kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba pamoja na
ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati.
13.Katika
mwaka 2015/16 jumla ya meta za ujazo wa miti zipatazo *767,946.46* zilivunwa
kutoka kwenye mashamba ya Serikali na kuingizia Serikali jumla ya Shilingi
*58,312,894,416.20*
14.Mapato
yanayotokana na zao la mbao,ni wastani wa Shilingi *Bilioni 18.3* kwa mwaka.
*Imeandaliwa
na Idara ya Habari-MAELEZO*
|
No comments:
Post a Comment