Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema anazipenda
Taasisi zinazofanya kazi ya kuonekana na sio zinazoongea ongea.
|
Akihutubia hapo Jana July 10, 2017 katika makabidhiano ya
nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation zitakazotumika katika
sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera, Rais Magufuli licha ya
kuipongeza Taasisi ya Mkapa akisema…“Mimi nazipenda sana Taasisi zinazofanya kazi
kama hii ya Mkapa Foundation sio zinazotaka watoto wazae wakiwa shule. Taasisi
za kila siku kwenye majukwaa mzinyime fedha, nataka Taasisi zinazofanya kazi
inayoonekana sio za kuongea ongea tu.
‘Hata mimi
yupo mtoto wa mdogo wangu amezalia nyumbani, mtoto anamuita John, wa pili
anamuita Samia lakini hakubakwa. Tunafanya ukaguzi nchi nzima kuwajua
waliotumia vibaya fedha za pembejeo ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.5.” –
Rais Magufuli.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50
zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
|
No comments:
Post a Comment