Mmoja wa
washiriki katika kongamano hilo, Joseph
Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine
ni Robert Madziva- Maxcom Africa
(kulia) na Chambi Chachage wakiwa
katika mjadala huo.
Kampuni ya
Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa
kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la
kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini
Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano
pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia
huduma hizo.
|
Mmoja wa
washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia)
akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka
kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na
Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo.
|
Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Jamii Media, Asha
Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii
Media, Maxence Mello alisema
kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala
mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa
watumiaji.
Alisema
wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za
kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za
maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma za
ICT.
Alisema
wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya
Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni
jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika.
Mkurugenzi
huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau
mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na
uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.
|
Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka
‘Compass Communications Ltd’ akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo.
|
Mmoja wa
washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose
Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT
kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert
Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo....SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.
Jiunge
nasi kwenye Social Media.
|
No comments:
Post a Comment