Wakati Leo Jumanne Juni 20, 2017
itakuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wagombea 62 tayari
wamejitokeza.
Wanafamilia hao ni wale
waliojitokeza kuanzia Ijumaa iliyopita Juni 16, mwaka huu wakiongozwa na Jamal
Malinzi aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu kati ya wagombea tisa walioomba
nafasi hiyo.
Fomu hizo zinachukuliwa na
kurejeshwa katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam na Uchaguzi wa TFF
utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.
Mbali ya Malinzi, wengine waliochukua fomu
hizo ni Imani
Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick
Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa
Rais wako Mulamu
Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa
kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:
Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na
Geita;
Soloum Chama
Kaliro Samson
Samwel Daniel
Leopold Mukebezi
Abdallah Mussa
Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;
Vedastus Lufano
Ephraim Majinge
Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na
Simiyu;
Benista Rugora
Mbasha Matutu
Stanslaus Nyongo
Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na
Manyara;
Omari Walii
Sarah Chao
Peter Temu
Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na
Tabora;
John Kadutu
Issa Bukuku
Abubakar Zebo
Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na
Rukwa;
Kenneth Pesambili
Baraka Mazengo
Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya na
Iringa;
Elias Mwanjala
Cyprian Kuyava
Erick Ambakisye
Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na
Ruvuma;
James Mhagama
Golden Sanga
Vicent Majili
Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;
Athuman Kambi
Dunstan Mkundi
Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na
Singida;
Hussein Mwamba
Mohamed Aden
Musa Sima
Stewart Masima
Ally Suru
Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na
Morogoro;
Charles Mwakambaya
Gabriel Makwawe
Francis Ndulane
Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na
Tanga;
Khalid Mohamed
Goodluck Moshi
Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam;
Emmanuel Ashery
Ayoub Nyenzi
Saleh Alawi
Shaffih Dauda
Thabit Kandoro
Abdul Sauko
Peter Mhinzi
Ally Kamtande
Said Tully
Mussa Kisoky
Lameck Nyambaya
Ramadhani Nassib
Aziz Khalfan
GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.
- Rais TSHS 500,000/=
- Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
- Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-
SIFA ZA WAGOMBEA.
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne
(Cheti cha Elimu ya Sekondari).
- Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu
uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
- Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi
kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
- Awe na umri angalau miaka 25.
- Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha,
Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika
ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
- Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji
katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
- anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na
kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa
kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu
ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni
..……………………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA
|
No comments:
Post a Comment