Mwenyekiti
wa Yanga SC, Yussuf Manji amejiuzulu wadhifa
huo akidai kuwa anatoa nafasi kwa watu wengine kuiongoza.
Barua
iliyosainiwa na Yusuf Manji Mei 22, 2017 inaonesha kwamba Manji ameachia rasmi
nasasi ya uenyekiti wa klabu ya Yanga SC na makamu Mwenyetiki wa klabu hiyo
Clement Sanga atakuwa Mwenyekiti na kuiongoza klabu hadi hapo uchaguzi
utakapofanyika ili kumpata Mwenyekiti mpya.
Kwa mujibu
wa maelezo ya barua, Manji alifikia uamuzi wa kujiuzulu Mei 20 mwaka huu siku
ambayo Yanga SC ilitangazwa kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017.
Katika barua
hiyo, Manji amsema ameamua kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine nao
kushika uongozi ndani ya klabu hiyo.
HAPA CHINI ISOME BARUA YOTE.
|
No comments:
Post a Comment