
![]() |
Mchezo huo
wa pili wa Kundi B kati ya Mali dhidi ya Niger umemalizika
kwa Mabingwa watetezi Mali kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo
yamefungwa na nahodha wao Mohamed Camara na Hadji Drame wakati Niger
wameambulia goli moja lililofungwa na Habibou Sofiane.
Ushindi huo
wa Mali unawafanya kuwa sawa kwa point na Tanzania na kuwa sawa
kwa kila kitu kwa maana ya magoli ya kufunga na kufungwa, Tanzania wana
point nne wakifunga magoli mawili na kuruhusu moja sawa na Mali wakati Mali
na Angola na wenye wakisalia na point moja wakifanana pia kwa kila kitu,
Tanzania sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa mwisho
dhidi ya Niger.
Jumapili May
21, 2017, zitachezwa mechi za mwisho za makundi na timu nne (mbili kutoka kila
kundi) zitasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
|
No comments:
Post a Comment