Jana
Jumanne,April 4, 2017 - Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura
kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.
Baada ya
mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job
Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchi.
Tanzania
inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza
washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na
hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.
Kati ya
wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama
cha Wananchi (CUF).
Wagombea wa
CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za
hapana.
|
No comments:
Post a Comment