![]() |
|
Katika mkoa
jirani wa Bubanza baadhi ya raia wameanza kuuza mabati ya nyumba zao ili waweze
kupata chakula.
Baadhi ya
viongozi tawala wamesema kuwa wana hofu ya kuzuka kwa wizi na vitendo vingine
viovu kutokana na njaa ambayo imeanza kubisha hodi katika mikoa hiyo.
Hivi karibu
baadhi ya raia wa mikoa ya Kayanza na Kirundo walikimbilia nchini Rwanda
kutokana na njaa ambayo imesababishwa na mashamba kuharibika kutokana na ukame.
"Tuna
hofu ya kuongezeka kwa visa vya wizi na hali hiyo huenda ikasababisha watu
kujichukulia sheria mkononi, ambapo mwezi akikamatwa anauawa. Hali hiyo huenda
ikasababisha kutokea kwa mauaji makubwa, " Jacques Nibizi, mkuu wa kijiji
cha Rukana ameonya. Kiongozi huyo amesema hivi karibu kuna mtu aliyeuawa
akijaribu kuiba.
Kwa mujibu
la gazeti la Iwacu, tayari viongozi tawala katika mkoa wa Cibitoke wameanzisha
zoezi la kuwatambua raia wanaokabiliwa na uhaba wa chakula pamoja na waathirika
wa majanga ya asili ili waweze kuwasaidia.
"Watu wanaohitaji msaada wa
chakula ni wengi na wengi ni kutoka wilaya za Buganda na Rugombo, "
kimebaini chanzo cha serikali ambacho hakikutaka jina lake litajwehuku
kikiongeza kuwa uhaba wa chakula unaweza kusababisha kulipuka kwa magonjwa kama
vile malaria na kipindupindu.
|
Thursday, February 02, 2017
Zaidi ya familia 300 zatoroka Makaazi yao kutokana na njaa mkoani Cibitoke/Burundi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment