Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Bw. Paul Makonda
amewataja Askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na Wafanya biashara ya Madawa ya
kulevya.
Aidha
amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na
kuwataka kuripoti kituo cha Polisi hapo kesho
February 03,2017.
Akiongea na
waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii,February 02,2017, RC Makonda amewataka wauzaji wote
kufika makao makuu ya Polisi kwajili ya kujieleza.
“Nimeamua
kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa
mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John
Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika
mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari
kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba
kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,”
alisema Makonda.
Aliongeza,’Wapo tuliowakamata
pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo
yanayotakiwa.
Lakini wapo
ambao bado, majina ni mengi sana mtayapitia wenyewe, kuna Mchafu, Director Joan, Mirror, Rommy na wengine wengi, wapo
wauzaji wadogo na wengine wakubwa.
Lakini wapo
wengine wanasemekana
wanatumia lakini hakuna ushahidi kwamba wanatumia ingiwa wenzao wanasema
wanatumia, ni bora nikakutana nao kesho pale Central, akiwemo TID, Wema Sepetu,”
List ya Watuhumiwa iko hapa Chini.
|
No comments:
Post a Comment