![]() |
Kete za
bangi 191 zikiwa zimekamatwa.
Jeshi la
Polisi Mkoani Kigoma limekamata Wahamiaji haramu 226, Kete za bangi 191, Heroin
kete tano , Pombe ya moshi lita 300 na silaha aina ya gobore moja, katika msako
wa kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji haramu pamoja na uhalifu uliofanyika
kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo salama.
Akitoa
taarifa ya Msako huo Jana February 17,2017, mbele ya Waandishi wa habari Mkoani humo , Kamanda wa
Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema kuanzia Februal 2 mwaka
huu jeshi la polisi Mkoani humo lilianza Msako wa kuhakikisha wanakomesha
vitendo vya uhalifu, matumizi ya Dawa za kulevya na uuzaji pamoja na wahamiaji
haramu wanaoingia Nchini bila vibali, hali inayo sababisha uhalifu kuongezeka
kutokana na vitendo hivyo.
Mtui alisema
kuwa mnamo februali 16 ulifanyika msako na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji
haramu 203 katika kijiji cha Mganza Wilayani Kasulu wakitokea nchini Burundi
wakiwa katika mashamba ya Wakulima,alisema na kuongeza kuwa Kigoma mjini
walikamatwa wahamiaji 7 , kibondo 9 na Buhigwe 7a na jumla yao ni wahamiaji 226
ambao waliingia nchini Kinyume na utaratibu huku wakipokelewa na Wenyeji na
wanawahifadhi.
Alisema
Wengi wa wahamiaji hao wanatoroka Nchini mwao wakiwa wamefanya uhalifu na
wanakuja Nchini na wanapokelewa na wenyeji na wanawatumia katika kilimo pia
wengi wao ndio wanaotumika kifanya uhalifu mkoani humo ambapo Kamanda Mtui
aliwaomba Wananchi kuacha kuwapokea Wahamiaji hao ambao wengi wao husababisha
madhala makubwa katika maeneo yao.
Aidha Mtui
alisema kwa upande wa madwa ya kulevya jeshi la polisi lilikamata katika Wilaya
ya Kigoma kete za bhangi 191 sawa na gram10 pamoja na Heroin kete tano, Kasulu
walikamata robo eka na gram 500 , kibondo miche 10 na Kakonko miche 60 ,kilo
moja ya Bhangi madawa hayo yalikuwa yakiuzwa kwa vijana ambao wengi wao
hawafanyi kazi na wanaendelea kufanya vitendo vya uhalifu.
"
tumeweza kutoa kipaumbele katika uhalifu unao tusumbua kwa kiasi kikubwa Mkoani
Kigoma ambao ni wahamiaji haramu , na matumizi ya Dawa za kulevya, kwa mujibu
wa upelelezi tulio ufanya wengi wanaoingia bila vibali ni wale wahalifu wanao
kimbia mikono ya sheria kutokana na uhalifu kama tunavyo fahamu muahalifu
hawezi kuacha uhalifu kiurahisi ndio ambao wanakuja kiendelea kufanya uhalifu.
....Niwaombe
Wananchi kuacha kupokea Wahamiaji halamu kwasababu kwa sasa tutakae mkamata
anawahifadhi wahamiaji halamu watafikisha mahakamani", alisema Kamanda
Mtui.
Alisema
katika msako huo zilipatikana idadi ya kesi katika msako huo ni kesi ya
uhamiaji haramu ni nane , kupatikana pombe ya moshi kesi 11, kupatikana Bhangi
kesi tisa , kupatikana na silaha kesi moja na kupatikana na heroini kesi moja,
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ilikuweza kujibu tuhuma zinazo
wakabili.
|
Saturday, February 18, 2017
![](https://1.bp.blogspot.com/-7Kd9qaiRHuA/WaEtZyc70TI/AAAAAAAADsA/7WUYBVoY-UwwjdEP3kDFPvH9htN0dDKgQCLcBGAs/s1600/demo-image.jpg)
Sakata Dawa za Kulevya Tanzania:Kigoma Nako kwa Tikisa.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment