Kamanda Sirro akizungumza na wanahabari leo February
10,2017.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru
atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda wa
kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa
hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Amesema
operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu
tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana
watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa
hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu
taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
|
No comments:
Post a Comment