Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka marais wastaafu kutokaa
kimya, badala yake wajitokeze kumshauri rais Magufuli wanapoona mambo hayaendi
sawa ili kunusuru nchi na uchumi.
Ameyasema
hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Isagehe,
Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
“Hii nchi
inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, nawaomba marais wastaafu wasikae kimya
kuhusu kunusuru nchi, wamshauri rais kuhusu mambo mbalimbali likiwemo la vyama
vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara,”amesema Zitto.
Aidha, Zitto
amemuomba rais Magufuli kufanya mabadiliko katika sekta ya madini kwa kuweka
wazi mikataba ya wawekezaji na kwamba jambo hilo litasaidia wananchi kuwa na
uelewa wa mikataba hiyo.
Hata hivyo,
Zitto ameshangazwa kuona barabara inayounganisha migodi mitatu ya dhahabu
ya Buzwagi, Bulyanhulu na Geita Gold Mine kuwa barabara hiyo haina kiwango cha
lami.
|
No comments:
Post a Comment