Akitoa
taarifa ya ajali ya basi la Mohammed Trans jana,January 08,2017, Kaimu Kamanda Polisi mkoani
hapa, Mayala Towo alisema ilitokea Januari 6, saa nne usiku katika Kijiji cha
Mseko wilayani Iramba.
Kamanda huyo
aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Mussa Rajabu (55), Farahan Manyama (34) na
John Tungaraza (39) wote wakiwa ni walimu, wakazi wa Geita.
Pia, alisema
majeruhi ambao pia ni walimu wamelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo.
Kamanda huyo
aliongeza kuwa walimu hao walikuwa wametokea kwenye Chuo cha Eckenford mkoani
Tanga walikokuwa wakichukua mafunzo mbalimbali. Alisema chanzo cha ajali hiyo
ni mwendo kasi wa dereva.
Towo alisema
basi hilo lenye namba za usajili T 786 AWJ aina ya Scania lilikuwa linaendeshwa
na Jovin Jackson (38), mkazi wa Shinyanga liligonga kwa nyuma lori lenye namba
B.6705A lililokuwa likivuta tela B.0568A lililokuwa likienda Burundi.
Akifafanua,
alisema dereva wa basi alitaka kulipitia lori hilo, lakini alipogundua hataweza
aliamua kurudi ghafla kushoto na mwendo kasi aliokuwa nao alijikuta analigonga
lori hilo kwa nyuma.
Towo alisema
baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka na kukimbilia kusikojulikana.
Juhudi zinaendelea kumsaka ili afikishwe mahakamani.
|
Monday, January 09, 2017
Watu Watatu wafariki Katika Ajali ya basi Mkoani Singida
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment