Kombe la Mapinduzi 2017 : Leo Azam FC vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni …Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 02, 2017

Kombe la Mapinduzi 2017 : Leo Azam FC vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni …Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku).

Mashindano  ya Kombe la Mapinduzi  2017 ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, ambayo yalianza December 31,2016 kwa Mechi moja ya Kundi A, yameendelea huko Amaan Stadium, Zanzibar kwa Mechi nyingine mbili za Kundi A.

Katika Mechi ya kwanza Juzi Usiku, Timu pinzani huko Zanzibar zilipambana na Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0.
Katika Mechi ya kwanza ya Jana January 01,2017  iliyochezwa mapema, KVZ ya Zanzibar ilichapwa 2-0 na URA ya Uganda, ambao ndio Mabingwa Watetezi, na Usiku, Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba SC, walitinga Amaan Stadium na kushinda bao 2-1 kwa kucheza na Taifa Jang’ombe na Simba SC walipata Bao la Kwanza Dakika ya 27 ambalo Muzamil Yasin alifunga na kupiga la Pili Dakika ya 41 Mfungaji akiwa Juma Luizio.
Dakika ya 76, Lufungo wa Simba  SC alijifunga mwenyewe na kuipa Taifa Jang’ombe Bao na kufanya mchezo umalizike kwa magoli  2-1.

Ratiba ya Mapinduzi Cup 2017- January 02, 2017

Azam FC vs Zimamoto - saa 10:00 jioni

Yanga SC vs Jamhuri - saa 2:15 usiku

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad