Pichani ni Goli
la kwanza la Arsenal ,lililofungwa na mfaransa Oliver Giroud ndio lilikuwa
kivutio na stori kubwa kwa wapenzi wa soka la England, kwani lilionekana
kulijadili zaidi katika mitandao kutokana na style yake lilivyofungwa na
kufananishwa na lile la Henrikh Mkhitaryan wa Manchester United alilofunga dhidi ya Sunderland.
Jumapili ya
January 01,2017 Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea kwa michezo
miwili ambapo katika kiwanja wa cha Emirates ,Arsenal waliwakaribisha Crystal
Palace kucheza nao mchezo wa 40 katika historia ya vilabu hivyo toka
walipokutana kwa mara ya kwanza 27,January 1934 katika mchezo wa FA Cup,
Arsenal wakiwa nyumbani walipata ushindi wa goli 2-0, magoli yakifungwa na
Oliver Giroud dakika ya 17 na Alex Iwobi dakika ya 56.
Msimamo wa Ligi
Kuu England 2016/2017 baada ya Matokeo ya mechi za January 01,2017.
|
No comments:
Post a Comment