Kiungo wa
Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Shirikisho
la soka barani Afrika CAF, January 05 2017, Abuja Nigeria ilifanyika hafla ya
utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na tuzo hizo utolewa kwa wachezaji
waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura.
Mchezaji wa
timu ya taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England, Riyad Mahrez
alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.
Mahrez
ambaye alipata kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili
kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa
kupata kura 186.
Mahrez
mwenye miaka 25, aliisaidia tumu yake Leicester kushinda taji la ligi kuu soka
England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England
sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.
|
Kipa wa Timu
ya Taifa ya Uganda na Mamelodi Sundowns, Denis Onyango ameshinda Tuzo ya Mchezaji
Bora wa Afrika Mwaka 2016 kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Bara la Afrika.
|
Kikosi bora
cha mwaka cha Africa
|
Bakary Papa
Gassama wa Gambia ndio refa bora wa Mwaka.
|
Asisat
Oshoala ndio mchezaji bora wa kike wa mwaka.
|
Timu bora ya
Wanawake Africa.
|
Klabu bingwa
ya Afrika - Mamelodi Sundwons wameshind tuzo ya klabu bora.
|
Tuzo ya timu
bora ya Taifa Mwaka 2016 imechukuliwa na Timu ya Taifa ya Uganda.
|
Kelechi
Iheanacho ameshinda tuzo ya "Most Promisng Talent".
|
Kocha wa
Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane ameshinda Tuzo ya kocha Bora wa Mwaka.
|
Tuzo ya
Mchezaji Bora kijana imechukuliwa na Alex Iwobi.
|
No comments:
Post a Comment