Mwaka 2016,
takribani wagonjwa 446,285 waliugua malaria. Asilimia 24.5% ya wagonjwa
waliohudhulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa walikutwa na
Malaria.
Kwa Wilaya ya Missenyi wagonjwa wanaougua malaria wamepungua kwa
asilimia 54% kwa mwaka 2016, kwa watoto chini ya miaka 5 wagonjwa wamepungua
kwa asilimia 64% na kwa watu wazima asilimia 45%.
Hii imechangiwa kwa kiasi
kikubwa na upuliziaji wa dawa ya ukoko uliofanyika mwaka 2016. Alisistiza Mkuu
wa Mkoa.
Aidha Mkuu
wa Mkoa wa Kagera alitoa wito kwa wananchi wa Halmashauri za Wilaya za Bukoba
(Vijini) Ngara na Missenyi kutoa ushirikiano kwa maafisa wanaohusika na zoezi
hilo ili kila nyumba iliyopangiwa kunyuziwa dawa ya ukoko unyunyiziwe bila
kipingamizi chochote ili kufanikisha lengo lililokusudiwa la kutokomeza ugonjwa
wa Malaria.
Dk. Magesa
Mratibu wa Mradi wa TBT Associate alisema kuwa zoezi la upuliziaji wa dawa ya
ukoko mjumbani kwa mwaka 2017 inaanza rasmi tarehe 25.01.2017 kwa Halmashauri
za Wilaya tatu Bukoba Ngara na Miseenyi na litadumu kwa siku 24 na
litahitimishwa tarehe 21 Februari, 2017.
Aidha, nyumba 163,299 zinatarajiwa
kupuliziwa dawa hiyo na kikosi cha wapuliziaji 743.
|
Zoezi la
upuliziaji wa dawa ya ukoko majumbani litavihusisha vyombo vya Ulinzi na
Usalama ili kuhakikisha linafanikiwa vizuri kutokana na baadhi ya wananchi kuwa
na mitazamo tofauti au imani potofu juu ya dawa ya ukoko na kupelekea
kuwahamsisha wananchi kutotoa ushirikiano katika majumba yao yapuliziwe dawa
hiyo.
Wito kwa
wananchi wa Halmashuri za Wilaya za Bukoba, Ngara na Missenyi ni kutoa
ushirikiano ili kila nyumba iweze kupuliziwa dawa ya ukoko ili kupambana na maambukizi
ya ugonjwa wa malaria unaoenezwa na mbu.
Kama zoezi hilo litafanikiwa kwa
kiwango kikubwa ugonjwa wa malaria utatokomezwa na kuwaacha wananchi kufanya
kazi zao bila madahara yoyote ya mwili yanayosababishwa na ugonjwa wa malaria
|
No comments:
Post a Comment