Rais
Erdogan wa Uturuki akiongea na mwenyeji
wake Rais Magufuli wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 23, 2017.
|
Rais
Erdogan na mwenyeji wake Rais Magufuli
wakishuhudia ubadilishanaji hati baada ya kusaini baina ya mwenyekiti wa
Wafanyabiashara wa sekta binafsi Dkt Reginald Mengi na kiongozi wa msafara wa
wafanyabiashara wa Uturuki katika kongamano hilo.
PICHA NA
IKULU
|
Serikali ya
Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya
kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo
baina ya nchi hizo.
Mikataba
hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti,
viwanda, afya na ulinzi.
Akizungumza
mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo Jana January 23,2017, Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo
cha ukuaji wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara
na kimaendeleo baina nchini hizo.
Rais
Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu
ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa
miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni
kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza
uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Aidha, Rais
Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika
kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.
Rais
magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la
Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa
kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa
nchi hizo.
Kwa upande
wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina
ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na
fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli
ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.
Rais Erdogan
alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya
wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza
ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.
“Kiwango cha
Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo
lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500,” alisema Rais huyo.
Aidha Rais
Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga
mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.
Nae Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya
mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika
kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana
taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.
Prof.
Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia
uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini.
|
No comments:
Post a Comment