Algeria na Zimbabwe waaga AFCON 2017-Leo Jan 24 ni Morocco v­­ Ivory Coast,Togo v Congo DR. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 24, 2017

Algeria na Zimbabwe waaga AFCON 2017-Leo Jan 24 ni Morocco v­­ Ivory Coast,Togo v Congo DR.

Hapo Jana usiku January 23, 2017,Michezo ya Kundi B ya michuano ya AFCON 2017 imeendelea kwa michezo miwili kuchezwa, huku Timu ya taifa ya Tunisia ambayo ilikuwa inahitaji ushindi ili kusonga mbele ilicheza dhidi ya Zimbabwe katika uwanja wa Stade de Amitie mjini Libreville.

Kufuatia ushindi wa Tunisia wa magoli 4-2 unawafanya wafuzu kucheza hatua ya robo fainali wakiungana na Senegal ambao ni vinara wa Kundi B.

Katika mchezo huo, magoli ya Tunisia yakifungwa na Naimu Sliti dakika ya 9, Youssef Msakni dakika ya 22, Taha Khenissi dakika ya 36 na Wahbi Khazri dakika ya 44, wakati magoli ya Zimbabwe yamefungwa na Knowledge Musona dakika ya 43 na Tendai Ndoro dakika ya 58.
Nao Algeria waliingia uwanjani kucheza na Senegal wakiwa wanahitaji ushindi huku wakiiombea mabaya Tunisia ambayo ilikuwa inacheza na Zimbabwe na  Algeria walilazimishwa sare ya 2-2 na Senegal.

Magoli ya Algeria yalifungwa na staa wao anayeichezea Leicester City ya England Slim Slimani dakika ya 10 na dakika ya 52 lakini magoli ya Papa Diop dakika ya 44 na Musa Sow dakika ya 53 yaliufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2 na kuifanya Algeria iage michuano hiyo bila kupata ushindi wowote.

Jumanne Januari 24,2017.

Kundi C

2200 Morocco v­­ Ivory Coast

2200 Togo v Congo DR

Jumatano Januari 25,2017.

Kundi D

2200 Egypt v Ghana

2200 Uganda v Mali

Robo Fainali

Jumamosi Januari 28,2017.

1900 Burkina Faso v Mshindi wa 2 Kundi B

2200 Mshindi Kundi B v Cameroon

Jumapili Januari 29,2017.

1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D

2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad