Rais wa 45
wa Marekani, Donald Trump pamoja na familia yake wakifurahia mara baada ya
kumaliza kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani,ma hapa chini akihutubia taifa kwa
mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Taifa hilo.
|
Rais wa
Marekania (Pichani) Donald Trump
ameanza kutia saini maagizo ya rais ,baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale
yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak
Obama.
Muda mfupi
baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bwana Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi
kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu
inayofahamika kama Obama Care, ambayo Trump
aliahidi kufanyia marekebisho.
Trump pia
ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa
kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.
Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho
mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa
kipaumbele na uongozi huo mpya.
|
Rais wa 45
wa Marekani, Donald Trump(mwenye tai nyekundu) akimsindikiza rais aliyemaliza
muda wake Barack Obama pamoja na aliyekuwa Makamu wa rais wake.
|
Baadhi ya
wananchi waliokuwa wanashuhudia kuapishwa kwa Donald Trump.
|
Rais wa
Marekani, Donald Trump akipeana mkono na rais aliyemaliza muda wake Barack
Obama.
|
Rais
aliyemaliza muda wake Barack Obama akiwapungia mkono.
|
Herikopta iliyombeba rais aliyemaliza muda wake Barack
Obama pamoja na mke wake ikiondoka.
|
No comments:
Post a Comment