VPL 2016/2017: Yanga SC yaisogelea Simba SC baada ya Kuifumua Ndanda FC 4-0. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Wednesday, December 28, 2016

demo-image

VPL 2016/2017: Yanga SC yaisogelea Simba SC baada ya Kuifumua Ndanda FC 4-0.

.com/simgad/
1
Mfungaji wa mabao mawili ya Yanga leo, Donald Ngoma (katikati) akimpongeza Amissi Tambwe baada ya kufunga bao la tatu.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Soka Vodacom Tanzania bara,Yanga SC Leo (December 28,2016) Jijini Dar es Salaam wameitandika Ndanda FC Bao 4-0 katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, na kujikita zaidi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba SC.

 Simba SC wana Pointi 41 kwa Mechi 17 na Yanga SC Pointi 40 kwa Mechi 18.

2
Hadi Mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele 3-0 kwa Bao 2 za Mzimbabwe Donald Ngoma, Dakika za 4 na 21, na Amissi Tambwe, 25, na Kipindi cha Pili kuongeza moja kupitia Vincent Bossou, 89.

Kipigo hiki kimeitupa Ndanda FC Nafasi ya 13 wakiwa na Pointi 19 kwa Mechi 18.

Katika Mechi nyingine iliyochezwa Leo,  Mtibwa Sugar waliiwasha Majimaji FC 1-0 huko Manungu, Morogoro.

Matokeo hayo yameipandisha Mtibwa Sugar hadi Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 30 kwa Mechi 18 na kuiacha Majimaji FC Nafasi ya 14.

Nafasi ya 4 inashikiliwa na Kagera Sugar wenye Pointi 28 kwa Mechi 17 na wa 5 ni Azam FC wenye Pointi 27 kwa Mechi 17.

Alhamisi zipo mechi 2 za VPL na moja ipo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Ruvu Shooting na Simba SC na nyingine ni pia Jijini Dar es Salaam huko Azam Complex kati ya Azam FC na Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *