Simba SC yapoteza Mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, December 12, 2016

demo-image

Simba SC yapoteza Mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar.

.com/simgad/
IMG_0012
Timu ya Mtibwa Sugar imepata ushindi  dhidi ya Simba SC, baada ya kuichapa mabao 2-1  jioni ya leo,December 12,2016 katika mchezo wa Kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mtibwa Sugar ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza tu ya mchezo huo, mfungaji Stahmili Mbonde aliyefumua shuti kali lililompoita kipa mpya kutoka Ghana, Daniel Agyei baada ya kufanikiwa kuwapiga chenga mabeki wa Simba SC.

 Mtibwa Sugar ikafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 34 mfungaji Jaffari Salum aliyewapiga chenga mabeki wa Simba SC baada ya kupokea pasi nzuri ya Ally Shomary na kumchambua Agyei tena.

Dakika mbili baadae Simba SC wakapata bao, dakika ya 36 lililofungwa na kiungo wa zamani wa Mtibwa, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim kwa shuti la kushitukiza lililompita kwa urahisi, kipa Said Mohammed aliyekuw amezubaa.

Kwa timu zote mchezo huo ulikuwa wa maandalizi ya mzunguko wa pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaoanza wiki ijayo,December 17,2016 kwa Simba SC wakifungua dimba na Ndanda FC mjini Mtwara na Mtibwa Sugar wakianza na Ruvu Shooting.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *