Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC Mchezaji bora Afrika 2016. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, December 12, 2016

demo-image

Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC Mchezaji bora Afrika 2016.

.com/simgad/
1

Riyad Mahrez baada ya kupokea tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2016

Mchezaji wa Timu ya Leicester City ya Uingereza , Riyad Mahrez ametawazwa kuwa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC wa Mwaka 2016.


Mashabiki kutoka kila pembe ya dunia walimpigia kura nyingi kiungo huyu wa kati wa Algeria na Leicester kuliko Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.
 

Mahrez ameambia BBC Sport: "Naam, [tuzo hii] ina maana kubwa sana kwa sababu bila shaka mimi ni Mwafrika na ni jambo kuu sana kwa mchezaji wa Afrika nafikiri, kwa hivyo nina furaha isiyo na kifani, najivunia kuipokea.."
2

Mahrez na kocha wake Leicester Claudio Ranieri.

Ni ufanisi mkubwa kwa mchezaji huyu aliyeanza maisha akicheza soka katika barabara za mtaa alipokuwa mtoto ambaye sasa amekuwa nyota anayeshindana na wachezaji bora zaidi duniani katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Amefunga mabao manne katika mechi tano alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ishara kwamba anaweza kutamba hati katika ligi zenye ushindani mkubwa zaidi.

3

Mahrez akiwa na mwanahabari wa BBC Peter Okweoche

Kadhalika, ufanisi wake umetambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA, ambao walimuorodhesha kwenye orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani - Mwafrika pekee katika orodha ya wachezaji 23.

Mahrez sasa anajiunga na vigogo wa soka Afrika , wakiwemo Abedi Pele, Jay-Jay Okocha na Didier Drogba, ambao wamewahi kushinda Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka.

Na ikizingatiwa kwamba bado ana miaka mingi ya kucheza, bado kuna muda kwake Mahrez kuwafurahisha mashabiki, ambao wameonesha jinsi wanavyompenda.Kusoma zaidi Profile na Habari kuhusu Mahrez-Bofya Hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *