Tetemeko lenye ukubwa wa Richa 7.8 limetokea katika eneo la
Cheviot Kaskazini mwa Christchurch huko New Zealand na kuua watu wawili,
imeripotiwa kutokea Tetemeko lingine nchini humo lenye ukubwa Richa 6.3 katika
eneo la South Island.
Tetemeko
hilo limetokea leo Jumatatu November 14, 2016 umbali wa maili 60 kutoka eneo
Christchurch, baada ya tetemeko lingine lilikuwa na mgandamizo wa Tsunami
kuipiga New Zealand usiku wa kuamika Jumatatu.
Kwa mujibu
wa Waziri Mkuu wa New Zealand John Key amethibitisha kutokea kwa matetemeko
hayo na vifo vilivyotokea, huku idara ya majanga nchini humo ikiwataka raia
wake kuhamia maeneo ya juu ili kujikinga na madhara yatakayotokea na bado
wanafanya uchunguzi kujua madhara ya kibinadamu na miundombinu yaliyotokea.
New Zealand
inatajwa kuwa katika eneo lenye mgandamizo mkubwa miamba ambayo hukatika au
kupasuka kutokana na kuwa karibu na bahari ya Pacific Ocean ambayo hukumbwa na
vimbunga vya Tsunami.
New Zealand
iliwahi kupigwa na tetemeko kubwa mwaka 2011 katika eneo la Christchurch na
kuua watu 185.
Hapa chini
Ni Picha Kadhaa zinavyoonesha Madhara yaliyotokea baada ya matetemeko hayo
kutokea nchini New Zealand leo Jumatatu Novemba 14,2016.
|
No comments:
Post a Comment