Makamu wa Rais Tanzania Asafiri kwa Ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 14, 2016

Makamu wa Rais Tanzania Asafiri kwa Ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Abiria waliokuwemo ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400  kabla ya kusafiri na Ndege hiyo kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016.

Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeendelea na hatua yake ya kupunguza matumizi baada ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kusafiri na msafara wake kwa ndege ya ATCL.

Safari hiyo ambayo ilihusisha maofisa 16 wa Serikali  imegharimu Sh7.6 milioni badala ya Sh40 milioni ambazo zingetumika kukodi ndege.

Akizungumza kabla ya kupanda ndege hiyo, Samia amesema ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha huduma za ATCL.

"Nimeamua kusafiri na ndege hii pamoja na msafara wangu huu ili kuunga mkono juhudi za Serikali yetu kwa ATCL, pia uzalendo na kupunguza gharama za matumizi hapa tungesafiri kwa ndege ya kukodi tungetumia takribani Sh40 milioni," alisema.

Samia alipanda ndege hiyo saa 9 jioni  alitarajiwa kuwasili Mwanza saa 10.20 jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo Novemba 14,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wakati akiindia ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad