AFRIM AWARDS Nigeria 2016: Diamond Platinumz ashinda tuzo 3, Awashukuru Mashabiki. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 08, 2016

AFRIM AWARDS Nigeria 2016: Diamond Platinumz ashinda tuzo 3, Awashukuru Mashabiki.

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul “Diamond Platnumz” ametoa shukrani zake kwa mashabiki wote waliofanikisha ajinyakulie tuzo tatu kutoka tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa juzi Jumapili jijini Lagos, Nigeria.

Tuzo alizoshinda staa huyo ni pamoja na WIMBO BORA YA MWAKA AFRIKA- UTANIPENDA, MSANII BORA WA AFRO POP AFRIKA na MSANII BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
Mbali na shukrani hizo, Diamond amewaahidi mashabiki wake wa Tanzania hususani wa jijini  Dar shoo kali katika mkesha wa X-Mass Desemba 24, mwaka huu ambapo atapiga shoo sambamba na vijana wake akiwemo RAYVANNY, RICH MAVOCO na HARMONIZE. 


Msanii wa Uganda Cindy Sanyu naye alijishindia tuzo la mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki huku Mwanamuziki Wizkid wa Nigeria akijishindia tuzo la msanii bora wa mwaka Afrika.

Tuzo ya Kolabo bora zaidi iliwaendea Eddy Kenzo na Niniola kutoka Nigeria
Mwanamuziki Wizkid wa Nigeria alijishindia tuzo la msanii bora wa mwaka Afrika.

Ifuatayo ni orodha ya wasanii walioshinda tuzo za Afrimawards:

1. Msanii bora wa kiume Afrika mashariki - Diamond Platnumz (Tanzania)

2. Msanii bora wa kike Afrika mashariki - Cindy Sanyu (Uganda)

3. Mwanamuziki bora wa Kiume Afrika Kusini - Black Coffee (Afrika Kusini)

4. Mwanamuziki bora wa Kike Afrika Kusini - Sally Boss Madam (Namibia)

5. Mwanamuziki bora wa kiume Afrika ya Kati - Wax Dey (Cameroon)

6. Mwanamuziki bora wa kike Afrika ya Kati - Bruna Tatiana (Angola)

7.Mwanamuziki bora wa kiume Afrika Kaskazini - DJ Van (Morocco)

8. Mwanamuziki bora wa kike Afrika Kaskazini - Zina Daoudia (Morocco)

9. Mwanamuziki bora wa kiume Afrika Magharibi - Flavour (Nigeria)

10.Mwanamuziki bora wa kike Afrika Magharibi - Aramide (Nigeria)

11.Mwanamuziki wa Kike mwenye ushawishi mkubwa - Naomi Achu (Cameroon)

12. Msanii bora wa bendi ya /Dou/GroupBand Afrika- Flavour (Nigeria)

13. Msanii anayeinukia vizuri zaidi - Amine Aub (Morocco)

14. Msanii anayependwa na mashabiki kote Afrika - Phyno (Nigeria)

15. Mtunzi wa Mwaka - Unique (Uganda)

16. Tuzo maalum ya utambulizi - King Sunny Ade (Nigeria)

17. Msanii bora /Duo/Group African Hiphop- Stanley Enow (Cameroon)

18. Msanii bora wa muziki wa rege na Dancehall - Patoranking (Nigeria)

19. Msanii bora wa muziki wa Utamaduni Afrika - Zeynab (Benin)

20. Msanii bora wa African Electro -Such (Zimbabwe)

21. Msanii bora wa Afrika katika RnB - Henok na Mehari Brothers (Ethiopia)

22. Msanii bora wa Afrika Muziki wa Rock -M'vula (Angola)

23. Msanii bora muziki wa muziki wa Jazz Afrika - Jimmy Dludlu (South Africa)

24. Kundi bora la muziki Afrika -VVIP (Ghana)

25. Kolabo bora Afrika - Mbilo Mbilo by Eddy Kenzo (Uganda) ft Niniola (Nigeria)

26. Video ya mwaka - Dogo Yaro by VVIP (Ghana)

27. Mwanamuziki Chipukizi wa Mwaka - Falz (Nigeria)

28. Albamu ya mwaka - Ahmed Soultan (Morocco)

29. Wimbo wa mwaka - Utanipenda Diamond Platnumz (Tanzania)

30. Msanii bora wa mwaka -Wizkid (Nigeria)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad