VPL 2016/2017- Mabingwa Yanga SC washindwa kupata goli dhidi Ndanda FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 07, 2016

VPL 2016/2017- Mabingwa Yanga SC washindwa kupata goli dhidi Ndanda FC.

IMG_0016

Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara ,umeendelea kuwa mgumu kwa Yanga SC baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mara nyingine kufuatia kulazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara ,leo Jumatano Septemba 07,2016.

Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda, Yanga SC walichezea kipigo cha goli 1-0 ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Ndanda FC kucheza dhidi ya Yanga SC ntangu walivyopanda daraja.
Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Ndanda FC

Matokeo hayo yameendelea kuzifanya timu hizo huongeza idadi ya michezo waliyotoka sare. Ndanda FC na Yanga SC zimeshakutana mara 5 hadi sasa, Yanga SC imeshinda mechi moja sawa na Ndanda FC ambayo nayo imeshinda mechi moja huku timu hizo zikiwa zimetoka sare michezo mitatu.

Ndanda FC ikiwa inacheza mchezo wake wa kwanza kwenye uwanja wa nyumbani iliweza kuhimili mashambulizi ya Yanga SC ambayo pia ilikuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza ugenini tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2016-2017. 


PICHA ZA MECHI YA YANGA SC NA NDANDA FC-BOFYA HAPA KUTAZAMA ZAIDI.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad