VPL 2016/2017-Azam FC wainyuka 1-0 Tanzania Prisons. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 07, 2016

VPL 2016/2017-Azam FC wainyuka 1-0 Tanzania Prisons.

Klabu ya Azam FC wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi kuu uliofanyika leo September 07,2016 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 Azam FC walipata goli dakika ya 59 baada ya kiungo wa timu hiyo Muivory Coast Kipre Bolou kupiga shuti kali lililogonga mwamba akiwa ndani ya eneo la hatari na kutinga wavuni.

Kwa matokeo hayo, Azam FC wanafikisha pointi 7 baada ya kucheza michezo mitatu sambamba na Simba SC na Mbeya City lakini timu zote zikitofautiana kwa wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad