Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara September 07,2016 - Simba SC yatungua 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 07, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara September 07,2016 - Simba SC yatungua 2-1.


Wekundu wa Msimbazi –Simba SC wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya  Ruvu Shooting katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jioni ya leo Jumatano Septemba 07,2016.

Iliwachukua dakika saba Ruvu Shooting kuwafunga Simba SC bao lililowekwa kimiani na Abraham Mussa kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Vicent Angban baada ya mabeki wa Wekundu hao kuzembea kuondoa hatari.

Kikosi cha Ruvu Shooting kilichoanza mchezo wa leo September 07,2016.

Kikosi cha Simba SC kilichoanza mchezo wa leo September 07,2016.. 


PICHA ZAIDI ZA MECHI YA SIMBA NA RUVU SHOOTING BOFYA HAPA.


Dakika tatu baadae Ibrahim Ajib aliisawazishia Simba SC kufuatia pasi safi iliyopigwa na winga Shiza Kichuya upande wa kushoto wa uwanja baada ya Maafande hao kushindwa kujipanga vizuri.

Mshambuliai Mrundi, Laudit Mavuto aliipa Simba SC ushindi kwa bao la pili dakika ya 48 baada ya kupokea pasi nzuri ya Ajib ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Ruvu.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, awali ikishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC na baadaye kulazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad