Mkoa wa Kagera tangu mwaka1987 hadi
sasa hauna chuo cha (Vocational Educational and Training Authority, VETA) cha
ufundi isipokuwa kuna Kituo cha mafunzo
ya ufundi (Vocational Training Center) VTC Rwamishenye ambacho ni kimojawapo
kati ya vituo 27 vinavyomilikiwa na VETA chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi nchini.
Kutokana na VTC kagera kutokuwa na
uwezo wa kudahili wanafunzi wengi aidha, kuwa kituo cha mafunzo kisichokuwa na
wanafunzi wa kulala (bweni) na kupelekea wanafunzi ambao ni wa nje ya Manispaa
ya Bukoba kukosa elimu ya ufundi na kuishia mitaani baada ya kumaliza elimu ya
msingi na sekondari ndiyo sababu Serikali ya Tanzania iliamua kujenga chuo cha
kisasa Kagera ili kupunguza tatizo hilo.
Ni baada ya Serikali ya Awamu ya Nne
chini ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete
kuamua kujenga Chuo cha Kisasa cha Ufundi, Rais Kikwete aliiomba nchi rafiki ya China
kujenga chuo hicho na kupendekeza kijengwa mkoani Kagera.
Aidha Mhe. Rais Kikwete alitangza
uamuzi wa Serikali ya China kukubali kujenga chuo hicho cha Ufundi Stadi Mkoani
Kagera Wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa Kilimani
tarehe 04/11/2014 na kuipongeza Serikali ya China kwa kukubali ombi lake kwa
dhati.
Wananchi wa Mkoa wa Kagera hatuna
budi kuupokea mradi wa ujenzi wa chuo hicho kikubwa cha kisasa na kitakachotoa
elimu ya ufundi wa kisasa unaoendana na sayansi na teknolojia , pia na kutoa
ajira kwa wananchi wa mkoa wetu wakati wa ujenzi na mara baada ya kumalizika
kujengwa kwa chuo hicho.
Na: Sylvester Raphael/KAGERA.
|
No comments:
Post a Comment