Huu umekuwa
ni wimbo wa taifa kwa watumiaji wa Smartphone. Sawa, kuna vitu vingi vya
kufurahia lakini tatizo linakuja kwamba simu haikai na chaji sana. Inapokuja
kwenye PHANTOM 6, port yake ya Type-C 2.0 USB ina uwezo wa kuchaji simu yako
kutoka 0% mpaka 35% ndani ya dakika 10 tu.
Kamera ya mbele (13MP) + Kamera ya
nyuma (25MP)
Sasa hapo ni
mwendo wa kutwanga selfies na picha kali ukiwa na kamera zenye uwezo wa hali ya
juu mbele na nyuma. Picha hizi zenye ubora wa kipekee zinazoongeza rangi na
uhai kwenye matukio yako ya kukumbukwa huku zikikutoa mwakemwake kama vile
haujapatwa na jua.
Muundo wa Chuma
Habari
nilizozipata kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ni kwamba, TECNO Phantom 6
itakuwa na ‘kava’ la chuma lilitengenezwa kwa umahiri wa hali ya juu na watu
wanaoipenda kazi yao.
Umbo Jembamba
|
Inasemekana
kuwa TECNO Phantom 6 itakuwa miongoni mwa simu nyembamba zaidi kutengenezwa
duniani. Yaani utafikiri aliyekuwa anabuni muundo alikuwa kwenye ‘diet’
Bei
Ingawa TECNO
Phantom 6 inategemewa kuwa ni miongoni mwa Smartphone zenye ubora wa hali ya
juu, wataalamu wa mambo wanasema kwamba bei yake haitapishana na mfuko wa
mwananchi.
Tusubiri
kuona zaidi maujanja ya Phantom 6, endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza
kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.
Twitter:
https://twitter.com/TECNOMobileTZ
|
No comments:
Post a Comment