Taswira Picha ya Matukio Bungeni Mjini Dodoma Leo Septemba 06,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 06, 2016

Taswira Picha ya Matukio Bungeni Mjini Dodoma Leo Septemba 06,2016.


Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 umeanza leo,Septemba 06,2016 mjini Dodoma, huku miswada sita ukiwemo wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa.

Katika mkutano huo, Wabunge wa kambi ya upinzani ambao walisusia siku kadhaa za mkutano uliopita, wamesema kwamba watahudhuria.

Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alithibitisha jana kwamba wabunge wa upinzani wataingia bungeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, Jumla ya maswali 110 yanatarajiwa kuulizwa na wabunge na kujibiwa na Serikali.

Aidha, Waziri Mkuu anatarajiwa kuulizwa maswali 16 ya papo kwa hapo. Taarifa hiyo ilisema Miswada sita ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Tatu wa Bunge na baadaye kupelekwa katika kamati husika ili ifanyiwe kazi, itaendelea kushughulikiwa katika hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na kusomwa kwa mara ya pili, kamati ya Bunge zima na kusomwa kwa mara ya tatu.

Miswada hiyo ni pamoja na ule wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Utathmini na Usajili wa Wathamini wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serika wa mwaka 2016.

Pia utakuwepo Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ya mwaka 2016.
Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuendesha mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 06,2016 Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai Akiwaongoza Wabunge wa kuimba wimbo wa Taifa wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa bunge wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 06,2016 Mjini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Selemani Said Jafo (MB) akieleza mpango wa kuendelea kuimarisha hospitali za Serikali Nchini.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akiwaeleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana,Wazee na Wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye  (MB) akieleza mipango ya Serikali katika kuimarisha michezo nchini na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidiana na Serikali  kuwekeza katika Michezo.       
Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe. Juma Nkamia akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (MB), wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad