Rais
mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akipokea heshima ya mizinga 21
kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini
Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa
Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016.
Rais
mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwa na mkewa Mama Esther Lungu
kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini
Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa
Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016.
Rais wa Zambia Edga Lungu ameapishwa
hii leo baada ya kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya
upinzani kushindwa katika kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa.
Mahakama ya katiba ilitupilia mbali
kesi ikisema kuwa upinzai ulikuwa umeishiwa muda wa kupeleka suala hilo
mahakamani.
Bwana Lungu alishinda uchaguzi wa
tarehe 11 mwezi Agosti kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichokwa kuepuka
kurudiwa tena kwa uchaguzi.
Rais
mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akila kiapo kwenye uwanja wa Taifa
wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za
kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia leo Septemba 13, 2016.
Bw.Hakainde Hichilema ambaye alichukua
nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo.
Inaelezwa kuwa takriban watu
60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Edga Lungu.
Taswira ya Makamu
wa Rais wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina akila kiapo ikionekana
kqwenye luninga kubwa kwenyeUwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka
leo Septemba 13, 2016.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akizungumza kwa niaba ya viongozi waalikwa wote.
Ndege vita zikipita angani.
Rais Edgar C. Lungu akielekea kukagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo.
Rais Edgar C. Lungu akikagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo.
Rais Edgar C. Lungu akielekea jukwa kuu baada ya kukagua gwaride la heshima .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na
viongozi walikwa wengine kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu
ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016.
Ndege vita zikipamba sherehe angani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akimpongeza Makamu wa Rais wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina kwenye
sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu
leo Septemba 13, 2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na
viongozi wengine wakisimama na kushiriki dua kwenye uwanja wa Taifa wa
Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka baada ya shughuli za
kuapishwa Rais Lungu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akinong'onezwa jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na
Maendeleo ya watoto Mhe. Agnes Musunga baada ya sherehe za kuapishwa kwa
Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akiongea na mwandhi wa habari wa ZNBC baada ya sherehe za kuapishwa kwa
Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment