|
Timu ya
Wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens wakiomba kabla
ya Mechi kuanza.
|
|
Kikosi cha
Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya
wanawake Burundi kilichoanza leo dhidi ya Kilimanjaro Queens.
|
|
Michuano ya
CECAFA ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati itafanyika kwa siku tisa
kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.
Kwa mujibu
wa CECAFA, Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu
kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda
na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja
na mwenyeji Uganda.
Tanzania
itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016 kabla ya kucheza
na Ethiopia Septemba 16, 2016.
Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, 2016
wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo,
Uganda itacheza na Kenya.
Michezo
mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza Septemba
13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, Kenya
itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa
kucheza na Burundi.
Nusu fainali
itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016
ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.
Mashindano
ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta
tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa
mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini
moja kwa moja tayari kwa safari ya Uganda.
|





No comments:
Post a Comment